Juventus imemsajili Alessandro Matri kwa mkopo kutoka Ac milan hadi mwisho wa msimu. Mshambuliaji huyo amerejea Turin baada ya Sebastian Giovinco ambaye aliondoka klabuni hapo jumatatu na kujiunga na Toronto fc.
Matri mwenye umri wa miaka 30 alifunga mabao 29 katika michezo 83 kati ya mwaka 2010 na 2013. Mapema January 2014 akapelekwa kwa mkopo Fiorentina kisha kupelekwa tena kwa mkopo klabu ya Genoa June mwaka jana. Msimu huu Matri amefunga mabao saba katika mechi kumi na sita.
0 maoni:
Post a Comment