Mwanamuziki
Ambwene Yesaya maarufu kama Ay ambae kwa sasa anatamba na ngoma kama
Touch Me amefunguka na kuweka wazi kuwa kujitoa kwao katika kundi la
East Coast Team lenye makazi yake Upanga mashariki kuwa pesa nayo
ilihusika licha ya
Ay
kutofautiana
na kutoelewana kimtazamo na mambo ya biashara ambayo ndiyoi yalipelekea
Ay na Mwana FA kujitoa katika kundi hilo ambalo kwa sasa lipo katika
mikakati ya kurudi kimuziki.
Ay alifunguka hayo jana alipotoa dakika 45 kwa mashabiki wake kumuuliza maswali kupitia Account yake ya Twitter aliyoipa jina la #ASKAY ndipo watu walitaka kujua chanzo cha wakali hao kujitoa katika kundi hilo la ECT ambalo lilikuwa likiongozwa na Gwamaka Kaihula (GK).
"Unahisi pesa ndio ilifanya EAST COAST kuvurugika?” Ofcoz ilihusika pia" lakini mbali na kutoa sababu ya pesa Ay alisema kuwa utofauti na kupishana katika mitazamo ilikuwa sababu nyingine kubwa wao kuondoka ila kuondoka kwao haikuwa na maana East Coast Team kuvunjika maana lilikuwa ni kundi na kulikuwa na watu wengi hivyo kundi kama kundi liliendela kuwepo ili hali wao walijitoa.
"kutoelewana kimtazamo na mambo Ya Biashara yalifanya tuondoke mimi na FA,ila si kama kundi lilivunjika"
Lakini Ay kupitia kipengele hicho ameweka wazi kuwa kwa sasa kuna kazi wamefanya na kundi la East Coast Team na siku za karibuni itatoka lakini amesisitiza kuwa wamefanya kazi na kundi hilo kama ambavyo wasanii wengine wanavyofanya nao kazi lakini haina maana kuwa wamerudi katika kundi
#AskAy hivi ni kweli Fa na Ay mmerudi East Coast Team ? @AyTanzania” hapana ila tunafanya nao Kazi kama artists wengine na mapaka sasa tumefanya kazi nao na Kazi itatoka very soon"
Mbali na kuzungumzia kundi la East Coast lakini pia mashabiki wa Ay walitaka kujua kuhusiana na mwanamuziki Amani ambae awali alikuwa akitambulika kama shemeji na Ay amesema kuwa katika mahusiano ya kimapenzi yeye na Amani yalikwisha muda mrefu na sasa amebakia kama rafiki wa kawaida na wanaowasiliana na kusaidiana ikiwa pamoja na kushauriana.
"Shemeji yetu amani umemwaga #AskAY” miaka mingi iliyopita sasa ni marafiki wa kawaida"
Ay leo anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Zigo na pia anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake mwingine mpya Its going down ambao kafanya na ms triniti pamoja na l'yamia.

0 maoni:
Post a Comment