Feb 2, 2015

ATLETICO MADRID WAISTUKIA PSG

Mabingwa wa soka nchini Hispania Atletico Madrid, wanajipanga kuwasilisha malalamiko yao FIFA baada ya kubaini njia za udanganyifu zilizokua zikifanywa na mabingwa wa soka kutoka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain dhidi ya Diego Pablo Simeone.
PSG wanadaiwa kutumia njia za kipuuzi kwa ajili ya kumrubuni meneja wa Atletico Madrid ili aweze kujiunga nao huko jijini Paris nchini Ufaransa kutokana na mwenendo wa meneja wao Laurent Blanc kutokua mzuri.
PSG wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kwa mara ya pili sasa na wamekua hawafanikiwi kutokana na Simeone kushikilia msimamo wake wa kutaka kusalia mjini Madrid huku akivujisha siri kwa viongozi wake.
Hata hivyo Atletico Madrid watakua na hoja ya kusikilizwa endapo watabisha hodi huko FIFA kwa kuwashtaki viongozi wa PSG kutokana mkataba wa Simeone uliopo hivi sasa ambao utafikia kikomo mwaka 2017.
Sheria zilizowekwa na FIFA duniani kote zinaikataza klabu yoyote kuzungumza na mchezaji ama kocha akiwa ana mkataba wa muda mrefu zaidi ya kufanya mawasiliano na viongozi wa klabu husika.
PSG wangekua na nguvu ya kuzungumza na meneja huyo menye umri wa miaka 44, endapo mkataba wake ungekua umesaliwa na muda wa miezi sita

0 maoni:

Post a Comment