Kiungo wa kati wa Manchester United
Angel Di Maria ndio mwathiriwa wa hivi karibuni wa wizi wa kutumia
mabavu nyumbani kwake huko Cheshire Uingereza, BBC imegundua.
Baadhi
ya wahalifu walijaribu kuvunja mlango wa nyumba yake katika barabara ya
Chelford huko Prestbury siku ya jumamosi jioni ,maafisa wa polisi wa
Cheshire wamesema.Hatahivyo mbiu ya mgambo ilipigwa kabla ya wezi hao kuingia ndani ya jumba hilo na kulazimika kutoroka.
Tukio hilo lilitokea baada ya Manchester United kuicharaza Leicester City mabao 3-1 katika uwanja wa Old Trafford.
0 maoni:
Post a Comment