Timu ya taifa ya Ivory Coast imekuwa timu ya nne kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Algeria .
Ivory Coast imeifunga Algeria kwa matokeo ya 3-1 katika mchezo ambao ulimalizika ndani ya dakika 90 .
Mabao ya Ivory yalifungwa na Wilfred Bony ambaye alifunga mabao mawili huku Gervinho akifunga bao moja .
Bao pekee la Algeria lilifungwa na Hilal Soudani kwenye kipindi cha pili .
Kwa matokeo haya Ivory Coast watacheza nusu fainali na Congo Drc huku Ghana wakicheza nusu fainali na wenyeji wa michuano hii Equatorial Guinea.
0 maoni:
Post a Comment