Shirikisho la mpira nchini Tanzania
(TFF) limesema kuwa kanuni haziruhusu kupata matukio ya ugomvi uwanjani
kwa kutumia ushahidi wa TV, redio au magazeti.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam, mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema
matukio mengi yanatokea uwanjani kwa mchezaji kufanyiwa faulo ya
makusudi au bahati mbaya, lakini ni vigumu kutoa uamuzi kwa ushahidi wa
kutegemea teknologia.“Wenzetu, kwa mfano chama cha mpira cha Uingereza (FA) wanaweza kufanya hivyo na kesi nyingi zimeamuliwa kwa ushahidi wa kutegemea video kwa sababu wana media centre yao.
“TFF kwa sasa hatuna media centre yetu inayohusu masuala ya
viwanjani ikiwa na vifaa vya kisasa, kwa hiyo tunategemea ripoti kutoka kwa kamishina wa mechi akiwa kama msimamizi ikiwa refa, msaidizi wake au washika vibendera (wasaidizi wa refa) hawajaona tukio”, alisema Wambura.
“Hatuwezi kuchukua sehemu ya mkanda wa mechi kutoka television binafsi au ya taifa kutafuta ushahidi kwani kwa sababu ya teknologia wanaweza kupunguza au kuongeza kitu katika kuhariri (editing), alisema Wambura.
Kauli ya Wambura inakuja huku kukiwa na matukio tata kadhaa yanayotokea katika ligi kuu ya wachezaji kuumia uwanjani na mashabiki wakiona hakuna hatua stahiki.
Miongoni mwa matukio tata ni la hivi karibuni ambapo mchezaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi alizimia uwanjani Jumapili iliyopita muda mchache baada ya kufunga goli dhidi ya Azam, kwa kile kinachodhaniwa na mashabiki wa Simba alipigwa kiwiko katika shingokwa makusudi wakati wa kugombania goli na refa hakuchukua hatua kwa mhusika kwa vile hakuona.
Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari kutoka Chama Cha Madaktari wa Michezo nchini (Tasma),wambao ndio wanatoa huduma ya kwanza uwanjani hapo, Richard Yomba, Okwi alizinduka muda mchache baade na kuelezea kuwa alihisi kupigwa kipepsi (na kiganja cha mkono) katika shingo kabla ya kuanguka.
Tukio kama hilo pia lilimkuta mchezaji Amisi Tambwe kutoka Uganda katika mechi ya ligi kuu alipodai kukabwa koo na mchezaji kutoka timu pinzani na vyanzo visivyoaminika vinadai yeye alianza ugomvi kabla ya kushambuliwa katika malipizi.
0 maoni:
Post a Comment