Feb 2, 2015

KOCHA SOUTHAMPTOM ATHIBITISHA KUSAJILI USIKU WA LEO

Koeman Athibitisha Kusajili Usiku Wa Leo

Meneja wa klabu ya Southampton ya nchini England Ronald Koeman, amesisitiza kufanya usajili angalau wa mchezaji mmoja kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa usiku wa kuamkia kesho.
Koeman alitoa uhakika huo jana jioni mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England ambapo Southampton waliaibika nyumbani baada ya kufungwa na Swansea City bao moja kwa sifuri.
Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amesema ameona kuna haja ya kufanya hivyo kufuatia uhitaji wa mchezaji mmoja katika kikosi chake ambacho kipo kwenye mikakati mizuri ya kuwania ubingwa msimu huu.
Wachezaji wanaohusishwa na mipango ya kusajiliwa na Koeman licha ya kutolewa msisitizo wa kusajiliwa mchezaji mmoja ni kiungo kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Feyenoord Tonny Vilhena pamoja na Filip Djuricic kutoka nchini Serbia ambaye anaitumikia klabu ya Benfica ya nchini Ureno.
Sababu kubwa ya Koeman kusisitiza suala la usajili wakati saa kadhaa zikisalia kabla ya dirisha dogo kufungwa ni kutaka kuziba pengo la kiungo Jack Cork, aliyempeleka kwa mkopo Swansea City.

0 maoni:

Post a Comment