Kocha mkongwe nchini, Abdallah
Kibadeni Mputa, ameanza kazi rasmi katika klabu hiyo katika nafasi yake ya
umakamu mwenyekiti wa kamati ya ufundi aliyoteuliwa.
Mwishoni mwa mwaka jana, Rais wa Simba, Evans
Aveva, alitangaza kamati mpya za klabu hiyo, akiwemo kocha wa zamani, King Kibadeni,
ambaye amepachikwa katika benchi la ufundi.
Kibadeni
amefunguka kuwa, tayari ameshaanza kuitumikia timu hiyo kwa kukutana na
viongozi wa Simba kwa kupanga mikakati mbalimbali kupitia mikutano, ikiwa na
lengo la kuisaidia Simba.
“Tayari tumeshakaa vikao viwili na viongozi wa
Simba lakini bado tunaangalia mechi zaidi, hivyo tutakutana tena na kamati ya
utendaji kwa lengo la kushauriana na kuona tunafanya nini kuisaidia timu yetu.
“Lengo letu ni kuona timu inafanya vyema kwa kuhakikisha wote tunakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuisaidia timu,” alisema Kibadeni.
0 maoni:
Post a Comment