Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola
amebadili uamuzi wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya bosi wake, Goran
Kopunovic kusisitiza: “Haondoki mtu.”
Habari za uhakika kutoka Simba zimeeleza,
Kopunovic aliutaka uongozi wa Simba kumuacha azungumze na Matola ambaye
aliueleza uongozi wa klabu hiyo ameamua kuondoka katika timu kubwa.
“Kweli, kocha alisema asingependa kumuacha
Matola ambaye amekuwa mchapakazi na mtu anayejua kuifanya kazi yake.
“Hivyo aliuomba uongozi azungumze na Matola
halafu atawapa jibu, kweli alifanya hivyo na mwisho wakaelewana.
“Hata baadhi ya viongozi nao walimfuata Matola
na kuzungumza naye kuhusiana na suala hilo na kumsihi abadili uamuzi,”
kilieleza chanzo cha uhakika.
“Nataka
nikuhakikishia, Matola hana tatizo, hata wale mashabiki waliomzomea hawajui
lolote. Viongozi wanaotaka maslahi ya Simba wanajua umuhimu wake na
anavyojituma.”
Alipotafutwa mwenyewe Matola, alipokea simu na
kusema: “Kwa sasa naomba mniache kidogo, nitalizungumzia vizuri siku nyingine.”
0 maoni:
Post a Comment