SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 29, 2016

BODABODA FC YATINGA NUSU FAINAL

Na Haji balou
Leo mei 29 kulikuwa na mchezo wa robo fainali mchezo ulipigwa ktk uwanja wa Shule ya msingi  muungano kati ya timu  Likongowele fc vs Bodaboda fc.

Mpaka mchezo unamalizika
Likongowele fc o-2 Bodaboda Magoli yote ya Boda Boda fc  yalifungwa na faraja katika dk 25 na dk 80

Mecho wa jana kati Vijuso fc vs kombaini fc  utarudiwa kesho jioni ndani ya dk 7 ikitokea sare zitapigwa penaiti.

May 28, 2016

NGASSA AITAJA TIMU INAYO MWITAJI VPL

Na Haji balou
Pamoja na uongozi wa Free State Stars
ya Afrika Kusini kumzuia kiungo wake
mshambuliaji, Mrisho Ngassa kumtoa kwa
mkopo, nyota huyo amewatoa hofu
mashabiki wa Yanga na kuwaambia siku si
nyingi anarejea kwenye klabu hiyo.

Ngassa ameitoa kauli hiyo muda mfupi
baada ya kuwasili nchini kisha kutazama
mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya
Yanga na Azam FC kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar ambapo Yanga ilishinda mabao
3-1.

Ngassa alijiunga na Free State inayoshiriki
Ligi Kuu Afrika Kusini, mwaka jana baada
ya mkataba wake kumalizika Yanga.
Ngassa amesema viongozi wa Yanga ndio waliowafuata Free State kwa ajili ya
kumuomba kwa mkopo ili aiongezee
nguvu timu hiyo katika hatua ya makundi
ya Kombe la Shirikisho Afrika.

NGASSA AITAJA TIMU INAYO MWITAJI VPL

Na Haji balou
Pamoja na uongozi wa Free State Stars
ya Afrika Kusini kumzuia kiungo wake
mshambuliaji, Mrisho Ngassa kumtoa kwa
mkopo, nyota huyo amewatoa hofu
mashabiki wa Yanga na kuwaambia siku si
nyingi anarejea kwenye klabu hiyo.

Ngassa ameitoa kauli hiyo muda mfupi
baada ya kuwasili nchini kisha kutazama
mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya
Yanga na Azam FC kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar ambapo Yanga ilishinda mabao
3-1.

Ngassa alijiunga na Free State inayoshiriki
Ligi Kuu Afrika Kusini, mwaka jana baada
ya mkataba wake kumalizika Yanga.
Ngassa amesema viongozi wa Yanga ndio waliowafuata Free State kwa ajili ya
kumuomba kwa mkopo ili aiongezee
nguvu timu hiyo katika hatua ya makundi
ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA TANGA BAADA YA TIMU ZAO TATU KUSHUKA DARAJA

Na Haji balou
KAIMU Katibu Mkuu wa Coastal Union,
Salim Bawazir amesema timu hiyo sasa
itakuwa chini ya usimamizi wa Nassor
Binslum pamoja na uongozi wa Chama
cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) kwa
ajili ya kuiwezesha kushiriki vyema Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ili irejee Ligi
Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti Bawazir
alisema: “Tumepata funzo kubwa,
kugawanyika kwetu ndiko
kulikotushusha daraja, sasa hatutakubali
mambo hayo tena, tutahakikisha Coastal
inashiriki kikamilifu Ligi Daraja la
Kwanza na msimu ujao tutarejea Ligi
Kuu Bara.”

Bawaziri alisema BinSlum na TRFA
watashiriki kikamilifu katika suala zima
la usajili wa wachezaji, kocha mwenye
ujuzi na uzoefu na kuilea timu ikiwa
kwenye kanda itakayopangiwa.

“Tunatambua kwamba FDL ni ngumu
kuliko hata ligi kuu ili uweze kufuzu ni
lazima timu iwe na mikakati kabambe
na si ubabaishaji,” alisema Bawazir.

May 27, 2016

WACHEZAJI AZAM FC WAPEWA MAPUMZIKO

WACHEZAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC, wamepewa
mapumziko ya wiki tano baada ya
kumaliza mechi ya mwisho ya msimu wa
2015/16 dhidi ya Yanga kwenye mchezo
wa fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam
Sports Federation Cup) juzi jioni.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya
NMB ambayo ni benki bora kabisa
iliyosambaa kila kona nchini, ilipoteza
mchezo huo wa fainali baada ya
kufungwa mabao 3-1.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu
Na mtandao huu mara baada ya
mchezo huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa
msimu ndio umeisha kwa timu hiyo na
kilichobakia ni kujipanga kwa ajili ya
kupata matokeo mazuri msimu ujao.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu
tumecheza mchezo wa fainali, ingawa
matokeo yalikuwa si mazuri haikuwa
malengo yetu, tulipanga kushinda lakini
lazima tukubali ni matokeo ya mpira,”
alisema.

Kawemba alisema wachezaji watamaliza
likizo hiyo Juni 30 mwaka huu na Julai
Mosi wataanza maandalizi ya msimu
mpya.
“Kwa hiyo tutafanya nini kwa msimu ujao,
tutamuongeza nani, tutamtoa nani hayo
tutazungumza baadaye lakini sasa hivi
tunawaomba washabiki wetu wawe
watulivu na tutaendelea kujipanga,”
alisema.

HAYA NDIO MASHINDANO MAPYA YANAYO DHAMINIWA NA AZAM TV

KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imeingia Mkataba na Shirikisho la
Mpira wa miguu Tanzania (TFF)
wenye thamani ya Sh.Bilioni 2 kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya Wanawake
Tanzania na Ligi Kuu ya Vijana wa
umri chini ya miaka 20.

Zoezi hilo limefanyika Ofisi za makao
Makuu ya Azam Media Ltd eneo la
TAZARA, Dar es Salaam upande wa
TFF ukiwakilishwa na Rais wake,
Jamal Malinzi na Azam Media
wakiwakilishwa na Mtendaji wake
Mkuu, Muingereza Rhys Torrington.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi,
Torrington amesema Mkataba huo ni
wa miaka mitano na lengo laoe ni
kuendelea kusaidia kuinua michezo
Tanzania.

"Baada ya mafanikio ya awali tukiwa
na Ligi Kuu ya Wanaume na
mashindano mengine, sasa tunapiga
hatua nyingine hatika jitihada zetu
kuchangia maendeleo ya soka nchini
kwa kuingia mikataba ya ligi hizi
mbili,"amesema Torrington.

Kwa upande wake, Malinzi amesema
kwamba Ligi Kuu ya Wanawake
itaanza kwa kushirikisha klabu 10
Agosti mwaka huu na Ligi ya U20
itashirikisha klabu zote za Ligi Kuu ya Wanaume.

"Na Ligi ya U20 itachezwa sambamba na Ligi Kuu ya wanaume, kabla ya mechi za timu za wakubwa,
zitatangulia mechi za vijana. Na kila
timu itasafirisha timu yake ya vijana
kwa mechi za mikoani. Itakuwa ligi
kamili na yenye kanuni
madhubuti,"amesema Malinzi.

MUSSA MGOSI ATAJA VITU VIWILI AMBAVYO HAWEZI KUVISAHAU MSIMU HUU

Na Haji balou
Mshambuliaji mkongwe wa Simba Musa Hassan Mgosi kupitia Simba news amesema kuna vitu viwili ambavyo hatavisahau baada ya msimu huu wa VPL kumalizika huku klabu yake ikiangukia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

“Kuna mambo mengi ambayo yametokea kwenye msimu wa 2015-16 lakini kwa upande
wangu, kuna vitu viwili ambavyo siwezi kuvisahau”, amesema Mgosi ambaye hakupata nafasi ya kutosha kucheza msimu huu kwenye kikosi cha Simba.

“Kitu cha kwanza ni mechi kati yetu ya nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Coastal Union. Coastal Union haikuwa timu ya kututoa sisi
lakini kwenye mpira hakuna udogo wa ukubwa wa timu inategemea na maandalizi ya timu, iliniuma sana kutolewa na timu kama Coastal”.

“Kitu kingine kilikuwa ni kufungwa mechi zetu zote mbili na watani wetu wa jadi Yanga, katika uwepo wangu Simba muda wote, hatujawahi
kufungwa na Yanga mara mbili mfululizo kwenye msimu mmoja, niliumia sana”.

May 26, 2016

ROBO FAINAL VIJANA CUP YAANZA RASMI LEO

Na Haji balou
Hatua ya robo final ya ligi ya mbuzi vijana cup imeanza Leo kwa mchezo mmoja kupigwa  katika uwanja wa Shule ya msingi muungano.

Mchezo huo ulikuwa ni kati ya wakaanga sumu fc  dhidi ya kigamboni fc Mchezo ulio malizika kwa wakaanga sumu kuibuka Na ushindi wa goli 2-1.

May 24, 2016

LIGI YA MBUZI VIJANA CUP YAMALIZIKA HATUA YA MAKUNDI KWA SIDO FC KUIBUKA NA USHINDI

Na Haji balou
Ligi ya Mbuzi Vijana cup imeendelea tena hii Leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika  uwanja wa shule ya msingi muungano katika kuhitimisha hatua ya makundi kati ya Sido fc dhidi ya Vijuso fc mchezo ambao umemalizika kwa Sido kuibuka Na goli 1-0.

Goli pekee la Sido fc lilifungwa Na Haikosi mpwate katika dakika ya 65 ya mchezo huo ligi hiyo itaendelea tena tarehe 26 mwezi huu kwa mechi za robo fainali.

Timu zilizoingia hatua ya robo final katika kundi A  Kigamboni, Kombaini, Mnalani, na Likongowele.

Kundi B ni Sido, Bodaboda, Wakaanga sumu na Vijuso.

YANGA KUPAMBANA NA TP MAZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Haji balou
YANGA SC imepangwa kundi la A
katika Kombe la Shirikisho Afrika
pamoja na mabingw awa zamani
barani, TP Mazembe ya DRC, MO
Bejaia ya Algeria na Medeama ya
Ghana.

Kundi B linaundwa na timu za
Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni  mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za  Morocco.

Mechi za mzunguko wa kwanza
zitachezwa Juni 17, mwaka huu na
Ratiba hiyo inamaanisha Yanga
itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC.

May 23, 2016

KIGAMBONI FC YAENDELEA KUTOA DOZII

Na Haji balou
Mchezo wa Ligi ya Mbuzi Vijana Cup imeendelea tena hii Leo Kwa Mchezo kati ya Kigamboni fc dhidi  Mnalani Mchezo ambao umemalizika Kwa Kigamboni kuibuka Na Ushindi wa goli 2-1.

Ligi hiyo inaendelea tena hapo kesho Kwa Mchezo mmoja kupigwa kati ya
Vijuso dhidi ya Sido mchezo utakao pigwa katika uwanja wa shule ya msingi muungano.

May 22, 2016

WAKAANGA SUMU WAPEWA POINT BILA KUTOKA JASHO

NA Haji balou
Ligi ya mbuzi vijana cup imeendelea tena leo  may 22 kwa mchezo mmoja kati ya kati ya Black star dhidi ya Wakaanga Sumu
Lakini timu ya Black star haikujitokeza uwanjani na haijatoa taarifa yeyote kwa uongozi wa Ligi .

Uongozi wa ligi unalazimika kutoa pointi tatu kwa timu ya Wakaanga Sumu kupewa ushindi wa goli tatu   na point 3.

Kesho kutakuwa na mchezo kati ya Kigamboni fc Vs Mnalani fc
Mchezo wa kesho unatarajia kuwa mchezo wa mkali kwakuwa Kigamboni wanataka kuendeleza kuweka rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote katika Ligi.

May 19, 2016

NANGANDO WAN'GAA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP

Na Haji Balou
Ligi ya mbuzi vijana cup Leo iliendelea ktk uwanja wa shule ya msingi Muungano kati ya Likongowele fc dhidi ya Nangando fc Mpaka dakika 90 zinamalizika Nangando fc imeibuka Na ushindi wa goli 4-2.

Magoli ya Nangando yalifungwa
Dakika ya 5 na Shehani Chikanga Dakika ya 10 na Ligubi Ligubi
Dakika ya 66 na Ligubi Ligubi
Dakika ya 87 na shehani Chikanga

Magoli ya Likongowele fc dakika ya 22 na Isihaka Haji dakika ya 65 na Faraji Manyai.

Baada ya mchezo kumalizika Abilah Rashid Kocha wa Nangando fc alisema kuwa ametumia mapungufu ya wapinzani wao katika mchezo wa leo Na hiyo Ndio sababu kubwaa ya wao kuibuka Na ushindi katika mchezo wa Leo.

May 18, 2016

SIDO FC YATOKA SARE DHIDI YA WAKAANGA SUMU KUBOTA NA ZFC ZAFUNGIWA

Na Haji balou
Mchezo kati ya Sido fc dhidi ya Wakaanga sumu umemalizika katika uwanja wa shule ya msingi muungano kwa sare ya goli 2-2.

Katika kipindi cha kwanza magoli ya Sido fc walifungwa namo dakika ya 7 na 15 yote yakipachikwa na Haikosi Mpwate na goli la Wakaanga Sumu likufungwa na  Bocho Shabani dakika ya 24.

Katika kupindi cha pili Wakaanga Sumu walisawazisha goli dakika ya 70 goli lililofungwa na Stamili Abduli
Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa Wakaanga sumu 2-2 Sido fc.

Nimezungumza na kamisaa wa mashindano ya ligi Shamte Mohamedi Shamte kuzungumzia sakata la mechi mbili za juzi kati ya Kubota fc Vs Kubota fc na Jana Z fc Vs Kigamboni fc kutokumalizika uongozi uliamua haya.

Timu zote ambazo zimeanzisha fujo katika mechi ya Jana Na juzii zimefungiwa katika mashindano hayo ya Kombe la mbuzi timu hizo ni Vijuso fc Na Zfc.

ORODHA YA TOP 10 WAFUNGAJI BORA ULAYA MESSI CHALIII

Na Haji balou
Luis Suarez (29) kwa mara ya kwanza alipata tuzo hiyo mwaka 2014 baada ya kufungana magoli na
Cristiano Ronaldo wakati huo akiwa Liverpool akifunga magoli 31 na kuwa mfungaji bora pia wa EPL.

Suarez amekuwa ni mchezaji wa kwanza La Liga mbali ya Messi na Ronaldo kushinda tuzo ya ufungaji bora tangu mwaka 2009.

Ukiwa msimu wa 2015-15 ukielekea ukingoni huku ukiwa umeisha kwa baadhi ya ligi, hii ndiyo orodha ya wafungaji 10 bora wa Ulaya msimu
huu:

CANNAVARO AMEFUNGUKA KUHUSU YEYE KUCHEZA TAIFA STARS KAMA ATAITWA NA MKWASA

Na Haji balou
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Nadir Haroub Cannavaro kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya Tanzania
kutokana na kuvuliwa unahodha bila kupewa taarifa rasmi, tuliwahi kusikia kocha wa Taifa Stars Boniface Mkwasa akisema kuwa bado Cannavaro yupo katika mipango yake.

Cannavaro amefunguka haya kuhusu yeye kucheza Taifa Stars kama kocha Mkwasa akimuita katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza na Kenya May 29 “Kwanza ieleweke sina tatizo na kocha Mkwasa hata kidogo ni kocha ambaye napenda kufanya nae kazai
akiniita nitamtafuta tutakaa chini kushauriana kiutu uzima halafu nitamwambia mimi naomba tu kwa
sasa niendelee kupumzika kuchezea Stars”

May 17, 2016

MASHABIKI WAANZISHA FUJO ZFC IKILALA 3-0

Na Haji balou
Mashindano ya kombe la mbuzi vijana yameendelea tena hii Leo kwa mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi muungano baina ya Zfc dhidi ya Kigamboni fc mchezo ambao hauku malizika kwa dakika 90.

Mpaka mchezo unavunjika Kigamboni fc ilikuwa inaongoza goli 3-0 magoli yaliyo fungwa Na Uwesu Mbala katika dakika ya 35, 65 Na 80.

Vurugu kubwa zilizo anzishwa Na mashabiki wa Zfc katika dakika za mwishoni  mwa mchezo wakidai mwamuzi wa Mchezo huo anawapendelea wapinzani wao.

May 16, 2016

VIJUSO FC YAICHAPA KUBOTA MECHI YAVUNJIKA

Image result for SPORTS
Na Haji balou
Mashindano  ya ligi ya Mbuzi vijana Cup yameendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Muungano kati ya Vijuso fc dhidi ya Kubota fc.

 Mchezo huo ambao haukumalizika baada ya kutokea fujo katika dakika ya 84, mpaka mchezo huo unavunjika tayari  Vijuso fc walikuwa wanaongoza goli 4-1 dhidi ya Kubota fc.

Baada ya mchezo huo kuvunjika kocha wa Kubota fc Ramadhani Ngazulu alitoa lawama zake kwa refa wa mchezo huo kwa kudai amewapendelea kwa kiasi kikubwa wapinzani wao na yeye ndio chanzo cha kuvunjika kwa mechi hiyo.

Lakini juhudi za kuwapata viongozi wa ligi hiyo hazi kufanikiwa na watatoa maelezo zaidi pale ambapo tutawapata pia watafafanua kanuni za ligi kuhusu mechi ikivujika hatua gani ambazo zinafuatwa.

May 15, 2016

KOMBAINI FC YAICHAPA LIKONGOWELE FC


Na Haji balou






Ligi ya Mbuzi Vijana Cup wilaya ya Liwale imeendelea tena hii leo  kwa mchezo mmoja kupigwa  katika uwanja wa shule ya msingi Muungano kwa Kombaini fc kuibuka na ushidi  wa  3-1 dhidi  ya  Likongowele fc.

Magoli ya Kombaini  fc yamefungwa na Mpilipili katika dakika ya  18 Sudi mbwana katika dakika ya 45 goli la mwisho limefungwa na zuberi zuberi dakika ya 65 goli la kufutia machozi kwa upande wa Likongowele fc limefungwa na Faraji Manyai katika dakika ya 25.

Baada ya mchezo kumalizika kapteni wa Likongowele Ramadhani mmango amesema kuwa kwa upande wao hawakucheza vizuri na timu yao ilikosa maelewano hasa eneo la kiungo.

Pia kocha wa Kombaini Haji mkutuma alisema mchezo ulikuwa mzuri lakini refa hakuwa katika upande wao ingawa wameibuka na ushindi wa goli 3-1 na malengo yao ni kushika nafasi ya kwanza katika kundi lao ili kusonga  mbele katika mashindano.

May 14, 2016

BODABODA FC YAICHAPA BLACK STARS

Image result for SPORTS
Na Haji balou
Timu ya Boda boda fc imeibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Black stars katika mchezo wa ligi ya Mbuzi ya Vijana Cup mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya  Msingi Muungano.

Magoli ya Boda boda fc yamefungwa dakika ya 27 kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji Abuu pia goli la pili lilipatikana kupitia kwa mchezaji Kazumali katika dakika ya 40 na goli la mwisho lilifungwagwa na Mbaraka masoud katika dakika ya 85  na goli la kufutia machozi kwa upande wa Black stars lilifungwa na Ally Omari katika dakika ya 20 ya mchezo.

Ligi  hiyo itaendelea tena hapo  kesho kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwaja wa Shule ya Msingi Muungano.

May 12, 2016

WAKAANGA SUMU WAICHAPA KUBOTA FC

Na Haji balou
Mpambano kati ya Kubota fc Na Wakaanga sumu fc  umemalizikaa kwa Wakaanga Sumu fc kuibuka Na ushindi wa goli 1- 0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Shule ya msingi Muungano.

Goli pekee la Wakaanga Sumu fc limefungwa Na Ema Ema katika dakika ya 60.

May 11, 2016

KIGAMBONI YA NG'AA VIJANA CUP

Na Haji balou
Timu ya Kigamboni fc yaendelea kung'aa baada ya kuibuka ushindi wa goli 1 bila dhidi ya Kombaini katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi muungano.

Goli pekee la kigamboni fc lililoipa ushindi lilifungwa Na Ramadhani mtunage Na katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza Na mpaka mchezo una malizika Kigamboni 1 Na Kombaini hawajapata kitu.

Ligi hiyo ya Mbuzi vijana cup inayoendelea wilayani Liwale itaendelea tena hapo kesho katika mchezo unao ikutanisha Kubota fc Vs Wakaanga sumu fc.

May 10, 2016

SIDO FC YAGAWA DOZI KWA BLACK STAR

Na Haji balou
Leo may 10 ligi ya Mbuzi vijana  Cup  imeendelea tena kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa shule ya  msingi muungano mechi kati ya Sido fc dhidi ya Black star.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu ambayo ilifanikiwa kuona lango la mwenzake lakii kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Sido ndio walikuwa wa kwanza kupata  goli kupitia kwa Haikosi mpwate katika ya dakika ya 65 dakika tisa baadae Festo Ashapira alifunga goli la pili dakika ya 80 Adam chonde aliipatia Black stars goli la kufutia machozi lakini dakika ya 85 haikosi mpwate aliiandikia Sido fc  goli la tatu mpaka mchezo unamalizika Sido fc 3-1 dhidi ya Black stars.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa sido fc Rajabu Mohammedi amesema pamoja na kupata ushindi mnono lakini wachezaji wake hawakucheza vizuri kutokana na kutofanya mazoezi ya kutosha.

Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho katika mchezo mmoja utakao ikutanisha Kombaini dhidi ya Kigamboni.


May 9, 2016

ZFC YAICHAPA NANGANDO FC

Na Haji balou

Ligi ya mbuzi Vijana Cup imeendelea tena hii leo katika mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi muungano kati ya Nangando fc dhidi ya Zfc na   umemalizika kwa Zfc kuibuka na ushindi wa goli 3-2.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wakusisimua Nangando fc  ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Shadhili lihambamba katika dakika ya 22 goli lililo dumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 50 Zfc walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mustafa Malunda lakini dakika tano baadae Nangando walipata goli la pili kupitia kwa Fadhili Mbwana mnamo dakika ya 70 Zfc walipata goli la kusawazisha kupitia kwa Mussa kisanga lakini Yahaya likule akamalizia msumali wa mwisho baada ya kuifungia Zfc goli la ushindi katika dakika ya 82.


Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Nangando Abduli ngeta  alisema wachezaji wake wamejituma lakini mpira ni mchezo wa makosa na bahati haikuwa kwao ndio maana wamepoteza mechi ya leo.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo kati ya Sido Fc dhidi ya Black stars 

May 8, 2016

BODABODA FC YAICHAPA VIJUSO FC BILA HURUMA



Timu ya Bodaboda fc imeibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Vijuso fc katika mchezo wa mashindano ya ligi ya mbuzi vijana Cup katika mchezo uliopigwa uwanja wa Shule ya Msingi Muungano.

Magoli ya Bodaboda fc yalifungwa na Saidi milasi dakika ya 40, Given ambaye alifunga magoli mawili katika dakika ya 60 na 67 na goli la mwisho lilifungwa na Bakari ng'ang'a huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Vijuso lilifungwa na Yuba mocha.

Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo mmoja kati ya Nangando fc dhidi ya Z fc mchezo utakao pigwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano.

May 7, 2016

LIKONGOWELE YAICHAPA MNALANI 4-3

Timu ya likongowele fc imeibuka na ushindi wa goli 4-3 dhidi ya Mnalani fc katika mchezo wa ligi ya Mbuzi Vijana Cup uliopigwa katika uwanja Shule ya Msingi Muungano.

Magoli  ya timu ya Likongowele yamefungwa na Twaha Tido katika  dakika ya 39,SelemaniMpoto katika dakika ya 47 na 60 huku goli la mwisho likifungwa Faraji Mayai na kwa upande wa Mnalani magoli yao yamefungwa na Imani Mohammedi aliyefuga goli mbili katika dakika ya 15 na 25 na goli la mwisho likifungwa dakika ya 74.



Katika mchezo wa leo mchezaji Abbuu Matwiko wa Likogowele fc na Abdulai ndandala wa Mnalani wameoneshwa kadi nyekundu katka dakika ya 85 baada ya kurushiaa matusi.

Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Mnalani Kasimu Malunga amesema kuwa walizidiwa nguvu na wapinzani wao lakini pia uzembe wa mabeki wake kushidwa kujipanga vizuri umesababisha wao kupoteza mchezo huo na wanajipaga kufanya vizuri katika mchezo ujao.

Pia kocha wa Likongowele Matisho Saidi amesema anamshukuru Mungu kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo na vijana wake wamefuata maelekezo aliyowapa mazoezini.

TAARIFA MPYA KUHUSU FARIDI MUSSA KUCHEZA ULAYA

Na Haji balou
Winger wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania Farid Musa amefaulu majaribio yake kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania ambako tayari pia amefaulu vipimo vya afya na kinachosubiriwa ni makubaliano kati ya klabu
hizo mbili ili kukamilisha deal.

Lakini nyuma ya pazia, kuna story kwamba wakalaambaye alitakiwa kusimamia kila kitu Farid anafanya majaribio akiwa nchini Hispania alilala-mbele kwa madai kwamba mteja wake hana vigezo ambavyo
alivitarajia.

Yusuf Bakhresa ambaye yupo Spain na Fafrid ameutonya mtandao huu  kuwa mawakala wengine ni wababaishaji baada ya wakala huyo kutimkia kusikojulikana na
kumuacha faridi kwenye ‘mataa’.

“Wakala John Sorzano aliyetakiwa kumsimamia Farid Musa kufanya majaribio nchini Hispania
alimtelekeza, baada ya Faridi kutua Hispania yule wakala akamtufuta mtu mwingine ili amsimamie Faridi.

Baada ya huyo wakala kumuona Faridi akaema hana viwango kwahiyo wote wakamtelekea”, anasema Yusuf ambay ilibidi avae majukumu ya kuhakikisha Farid
anapata nafasi ya kufanya amajariio kwenye klabu ya Tenerife.

“Kwa bahati nzuri mimi (Yusuf) nilikuwa hapa, ikabidi nianze kumtunza Farid. Nikafanya
mawasiliano na viongozi wa Tenerife wakakubali kumpa nafasi ya kuendelea kufanya majaribio,
baada ya Farid kuonesha uwezo mkubwa wakamkubali.

Wale mawakala wakapata taarifa
kwamba dogo amekubalika, waanza kuja kutaka kusimamia dili”.
“Mimi nimewapiga chini na nimeuambia uongozi wa Tenerife uandike barua rasmi kwa Azam.
Muda wowote watatuma offer kwa klabu ya Azam na kufanya bishara ya kumuuza Farid”.

May 2, 2016

TIMU YA LIKONGOWELE,SIDO FC ZATAMBA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP WILAYANI LIWALE

Mwandae Mchungulike


                                                     SIDO FC Vs BODABODA
                                                         SIDO FC Vs BODABODA
Timu ya SIDO FC Vs BODABODA 
LIWALE,Katika kundi A Jana mei mosi katika ligi ya Mbuzi vijana cup hapa wilayani Liwale ilitimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano zilikutanishwa timu ya Z.F.C Vs LIKONGOWELE katika kipindi cha kwanza timu ya Likongowele ilikuwa ya kwanza kujipatia goli namo dakika 45 lilofungwa na Twaha Tido na goli lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza mchakamchaka huku kila timu ikisaka goli katika dakika ya 85 timu ya Likongowele iliongeza goli la pili na dakika ya 87 waliongeza goli la tatu lililofungwa na Twaha Tido huku mwamuzi wa mchezo alipopuliza kipenga cha kumaliza mpira dakika 90 matokeo yalikuwa Z.F.C 0-3 LIKONGOWELE.
Kocha wa timu ya Z.F.C alisema wamecheza vizuri japo wamefungwa goli 3 kwake ni jambo la kawaida ni moja ya mcheza na kocha wa Likongowele Juma Mtumbatu alisema kitu kilisaidia kupata ushindi ni mazoezi na wachezaji wake ni watii sana kwa kile anachowafundisha.
Leo mei 2 katika kundi B kulikuwa na mchezo,mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano kati ya timu ya SIDO FC Vs BODABODA katika kipindi cha kwanza Sido fc ilioongoza goli 1 lililofungwa katika dakika ya 40 kupitia mchezaji wao Aikosi goli lililodumu mpaka mapumziko.
Dakika ya 49 ya kipindi cha pili timu ya Bodaboda ilisawazisha goli lililofungwa na Faraja na kupelekea mchezo kuwa mkali zaidi huku kila timu ikihitaji kuongeza goli la ushindi katika mchezo huo.
Namo dakika ya 81 timu ya Sido fc kupitia mchezaji wake Mohamedi alipachika goli la pili ambalo Bodaboda walitaka kusawazisha lakini ujanja ulikuwa mdogo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Bodaboda walikubali kichapo cha goli 2 kwa 1.Matokeo yalikuwa SIDO FC 2-1 BODABODA
Kesho mei 3 katika kundi A kutakuwa na mchezo kati ya timu ya MNALANI Vs KOMBAINI mchezo unaotarajia kuwa mkali wa aina yake kwani timu ya Mnalani iliweza kushinda bao 6 huku timu ya Kigamboni iliweza kuicha timu ya Likongowele bao 3 kwa 1.
KUANGALIA MATOKEO YOTE YA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP >>BOFYA HAPA