Feb 3, 2015

ALICHOSEMA NATURE KUHUSU WASANII WA ZAMANI


Nyota na msanii mkongwe wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Juma Nature amesema kuwa wasanii wakongwe wa muziki huo watapotea kabisa katika ramani ya muziki kama wadau wa muziki pamoja na vyombo vya habari havitawapa nafasi ya kutosha kama wanavyopewa wasanii wengine wa sasa.

Nature amesema kuwa zamani kipindi yeye yupo Bongo Records wasanii wote walikuwa kitu kimoja na kazi zao walikuwa wanafanya kwa kushirikiana na kwa umoja kitu ambacho kilifanya wote kuwa namafanikio sawa kwani hata maonesho yao walikuwa wanagawana fedha sawa kitu kisichowezekana kwa sasa.

Nature amesema kuwa kwa sasa wasanii kama yeye watapotea kutokana na wadau wa muziki kuwatumia wasanii wachache katika shughuri zao za kila siku huku akitolea mfano jinsi Diamond anavyopewa kipaumbele katika maonesho na kazi nyingine huku wasanii wazuri kama Rich Mavoko na Ali Kiba wakisahaulika kitu kinachosababisha kuwa na matabaka kwani wanaopewa nafasi ndio wanaofanikiwa.

Katika hatua nyingine Juma Nature amewaasa wadau wa muziki kutowasahau wakongwe wa muziki nchini kwani wao ndio walioufikisha muziki huu hapa ulipofika.

0 maoni:

Post a Comment