MABINGWA wa ligi kuu Tanzania
bara, Azam fc wamemaliza ziara yao nchini Congo DR ambako wameshiriki
michuano ya Mazembe inayoendelea mjini Lubumbashi.
Azam walianza kwa kufungwa goli
1-0 na TP Mazembe, wakatoka sare ya 2-2 na Zesco United ya Zambia na leo
wamefungwa 1-0 na Don Bosco.
Katibu Mkuu wa Azam fc, Idrissa
Nassor ‘Father’ amesema kikosi cha Azam kitatua kesho jijini Dar es
salaam tayari kwa maandalizi ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya
Polisi Morogoro itayopigwa uwanja wa Jamhuri mwishoni mwa wiki hii.
“Tutarudi kesho saa mbili
asubuhi, tutarudi Chamazi na kuendelea na mazoezi kuelekea mechi ya
jumamosi Morogoro dhidi ya Polisi Morogoro. Baada ya hapo tutacheza na
Mtibwa Sugar”. Amesema ‘Father’ na kusisitiza: “Mazoezi ya Congo
yalikuwa maalumu kwa mechi za ligi ya mabingwa, tumejifunza mengi na
tunatarajia kufanya vizuri”.
0 maoni:
Post a Comment