Feb 3, 2015

JACKLINE WOLPER AMKUBALI AY

Acctress Jacquline Wolper kutoka katika kiwanda cha filamu bongo amewataka watanzania kupenda kazi za wasanii wa nyumbani na kuwapa support katika kazi zao wanazofanya ili kuwatia nguvu na kuwapa moyo wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi kwa
Msanii Jacqueline Wolper
watanzania,Wolper amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Instragram alipokuwa akionyesha jinsi gani ameguswa na kazi mpya ya msanii Ambwene Yesaya (AY).
Wolper alisema kuwa katika maisha ya kila siku ni vizuri raha na burudani kupata na watu waliokuzunguka maana hao ndio msaada wako hata pale utapatwa na matatizo
"Jioni yangu ya leo(Jana) imekua nzuri sana nimemaliza kazi,mapema mbio nyumbani kuburudika na nyimbo mpya ya msanii ninayemkubali kaka Ay jamani tupende vya nyumbani na Raha pata nawalokuzunguka mimi na familia tuko happy nazigo tumeliewa sema nini nina kazi hii week nzima Radio itapasuka maana dada hata akiwa jikon atakua na usemi wa zigo zigo hahaha big up my broo we love u Ay"
Mwanadada Jackline Wolper ameungana na msanii Ommy Dimpoz kutibitisha kuwa Ay amefanya kazi nzuri na kali ambayo kwa matazamo wao wanaamini kuwa itafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari na hiki ndicho Ommy Dimpoz amefunguka
"Zigo jipyaa kotoka kwa Yesayaaaaa Ay hatariii sana naona kaamua kuchukua hela zake sasa"
Ay jana ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Zigo ambao umefanywa na Produza Narheel na kufanyiwa Mixing katika studio za Mj Records lakini pia mkali huyo jana ameachia Video ya wimbo wake wa It's going down.

0 maoni:

Post a Comment