MSHAMBULIAJI wa Totenham Emmanuel Adebayor alikuwa anajiandaa kuihama klabu hiyo katika siku ya mwisho ya usajili, Lakini ajabu mpango wake ulikwama dakika za mwisho.
Adebayor alikuwa anajiandaa kuhamia West Ham lakini Totenham walitangaza kuwa dili hilo limeshindikana na mchezaji huyo anabaki. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Spurs na msimu huu amefunga mabao mawili katika mechi kumi na tano.
0 maoni:
Post a Comment