Mwenyekiti wa kamati ya
usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemwambia kiungo mkongwe wa Simba,
Shabani Kisiga asidhani anausumbua uongozi wa klabu hiyo kwa kuondoka kambini.
Kisiga ameondoka kambini
Simba kwa madai amekuwa hachezeshwi, lakini Hans Poppe amesema anajipotezea
muda wake.
“Hawezi kutusumbua sisi,
aliwahi kutusumbua lakini alirudi na kusema kwamba sasa yuko vizuri.
“Kisiga alisema amekuwa
tofauti, lakini sasa ameamua kuondoka jambo ambalo halitusumbui na ingekuwa
vizuri afanye utaratibu aende tu kwa amani kuliko kufanya hivyo,” alisema.
Hans Poppe alisisitiza
suala la nidhamu huku akisema Kisiga alipaswa kuwa mfano katika suala la
nidhamu.
Pia alisema mwenye uwezo wa
kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran
Kopunovic asingemuacha nje.
Pia alisema mwenye uwezo wa kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran Kopunovic asingemuacha nje.
0 maoni:
Post a Comment