Kocha Mkuu wa Simba, Goran
Kopunovic ameonyesha wazi masikitiko yake kutokana na kifo cha ghafla ya Kocha
Jean Marie Ntagwabila.
Kopunovic amesema
amesikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa kocha huyo raia wa Rwanda alikuwa kati
ya rafiki na wapinzani wake kikazi.
“Wiki iliyopita nilikuwa
nafuatilia habari zake mtandaoni, kwa kweli imenisikitisha sana.
“Wakati nikiwa Polisi
Rwanda, alikuwa mpinzani wangu mkubwa akiwa na Kiyovu. Aliwahi pia kufundisha
timu nyingine za Rwanda kwa mafanikio makubwa,” alisema raia huyo wa Serbia.
Ntagwabila amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo baada ya kukimbizwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kanombe
jijini Kigali kutokana na matatizo ya mapafu yaliyosababisha ashindwe kupumua.
Simba iliamua kumchukua
Kopunovic baada ya kuona wanamhitaji zaidi ya Ntagwabila ambaye pia alikuwa na
nafasi ya kuchukua mikoba ya Patrick Phiri raia wa Zambia aliyetimuliwa Simba.

0 maoni:
Post a Comment