Kikosi cha Yanga, kimetua
salama mjini Tanga kujiandaa na mchezo wake wa kesho dhidi ya Coastal Union.
Lakini Yanga wamekataa
kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao walitakiwa kufanya mazoezi leo
na kuamua kufanya mazoezi kwenye uwanja wa jeshi.
Msemaji wa Yanga, Jerry
Muro amesema walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo na si Mkwakwani.
“Nafikiri hakuna tatizo,
kilichotakiwa pale ni suala la mazoezi na tumefanya, hivyo hakuna tatizo lolote,”
alisema Muro.
Yanga ina kibarua cha kuivaa Coastal Union kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
0 maoni:
Post a Comment