Harry
Redknapp ameachia ngazi Queens Park Rangers kufuatia maumivu ya magoti
lakini ameweka wazi kuwa bado huo hautakuwa mwisho wake wa kufundisha
soka.
Redknapp,
67, amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuambiwa kuwa atahitajika
kufanyiwa upasuaji wa magoti yake yote mawili. Hawezi kutembea hata
hatua 100, akakiri kuwa kwa sasa yeye si mtu sahihi wa kuiongoza QPR
katika vita vya kushuka daraja. Akampigia mmiliki wa timu saa 11.30
alfajiri na kumjulisha habari hizo.
Kocha
huyo mkongwe anasema: “Sikupata usingizi usiku mzima, nawaza kuhusu
hilo. Siwezi kutembea, nimekuwa kwenye maumivu muda wote. Nimejitahidi
sana lakini inafika hatua nakuwa siwezi kufanya kazi yangu.
“Siwezi kwenda uwanjani, hata kama gari litaniingiza mpaka ndani lakini bado nitapaswa kutembea kidogo.
“Nilikwenda
uwanjani kumtazama mjukuu wangu akicheza soka wikiendi iliyopita lakini
baada ya dakika tano tu nililazimika kurudi kwenye gari. Sikuweza hata
kusimama. Ni maisha gani haya kama huwezi hata kutazama watoto
wakicheza? Nikafikiria usiku kucha, baadae nikaamua kumipigia Tony
Fernandes.
0 maoni:
Post a Comment