Kwa ufupi
Maombi hayo yalisomwa kwenye kikao cha 24 cha marais
wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia na
ikapitishwa kwa kuundwa kamati maalumu ya kusimamia mashindano hayo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora alisema
jana kuwa klabu hiyo imejitolea kuchangia matibabu ya ugonjwa huo katika
nchi zilizoathirika.
Alisema mwenyekiti wake, Yusuf Manji atayadhamini mashindano kwa Dola 500,000 na kwamba yatajulikana kama, ‘Mashindano Huru ya Bara’.“Mwenyekiti wetu (Yusuf Manji) aliwasilisha dodoso kwenye Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikisha Serikali, kuandaa mchakato wa kuchangisha fedha kwa wafanyabiashara wakubwa kwa nchi wanachama wa umoja huo, lengo likiwa ni kuzisaidia nchi zilizoathirika na ugonjwa wa ebola. “Ni kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa Yanga, ambayo ni klabu kubwa na wenye mashabiki wengi Tanzania, mpira pia ni biashara, ikapendekezwa kupitia mpira pia kuwe na mashindano ambayo yatachangia waathirika wa ebola. Maombi hayo yalisomwa kwenye kikao cha 24 cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia na ikapitishwa kwa kuundwa kamati maalumu ya kusimamia mashindano hayo. Tibohora alisema mashindano haya yatashirikisha timu 108 kutoka kila nchi mwanachama wa AU, ambaye pia ni mwanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zitaingiza timu mbili, mshindi wa kwanza na wa pili hapa nchini timu watashiri
0 maoni:
Post a Comment