Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema hali ya kikosi chake kushindwa kutumia nafasi inachanganya, lakini hawataka tamaa.
Pluijm amekuwa akilia na nafasi nyingi wanazopoteza katika kila mechi.
"Kweli
bado ni tatizo, si dogo kwa kuwa kila mmoja anaweza akaliona sasa.
Tunahitaji kuendelea kulifanyia kazi, tunahitaji kutulia na hatuwezi
kukata tamaa.
"Ukisema
tukubali kuchanganyikiwa, tunaweza kujichanganya zaidi. Lakini ni
lazima tukubali kuna tatizo na lazima tulitatue," alisema Pluijm.
Wachezaji wa Yanga wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi katika kila mechi, hivyo kuifanya timu yao itoke bila mabao.
Mara
ya mwisho, Yanga imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda FC huku
washambuliaji wake wakipoteza nafasi takribani saba za wazi za kufunga.
0 maoni:
Post a Comment