Unamkumbuka
Yakubu yule mshambuliaji Mnigeria, amerejea England na kujiunga na Reading.
Aliwahi
kung’ara na Everton na Middlesbrough halafu akaamua zake kuondoka kwenda Qatar
na kujiunga na Al Rayyan.
Kocha Steve
Clarke wa Reading amesema wamemsajili kwa muda mfupi kama mchezaji huru.
Mnigeria huyo
imeelezwa ana miaka 32 ingawa muonekano wake unaonyesha ana zaidi
Mara ya kwanza, Yakubu alitua England akitokea Maccabi Haifa akajiunga na Portsmouth kwa mkopo, hivyo ilikuwa mwaka 2003.
0 maoni:
Post a Comment