Feb 3, 2015

KOCHA SIMBA AFRIKI DUNIA RWANDA


 
Na Mwandishi Wetu, KIGALI
KOCHA Jean Marie Ntagwabila aliyekuwa atue Simba SC Januari mwaka huu kuwa Msaidizi wa Mserbia, Goran Kopunovic katika klabu ya Simba SC amefariki dunia leo nchini Rwanda.
Ntagwabila amefariki ghafla katika hospitali ya Jeshi, Kanombe baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
Simba SC ilikuwa kwenye mchakato wa kumleta marehemu afanye kazi na Goran, lakini Mserbia huyo alimkataa na akapendekeza aletwe Mnyarwanda mwingine, Alphonse Gatera aliyekuwa Msaidizi wake wakati anafundisha Polisi ya Rwanda.
Marehemu atakumbukwa nchini Rwanda kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake, ikiwemo kuifanya APR iwe tishio mno kiasi cha kufikia kuifunga Zamalek ya Misri mabao 4-1 mwaka 2004 katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikitoka kufungwa 3-2 katika mchezo wa kwanza Cairo.
APR ilisonga mbele hatua ya 16 Bora, ambako ilikwenda kutolewa kwa mbinde na Africa Sports ya Ivory Coast kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake. Bwana ametoa, bwana ametwaa. Pumzika kwa amani Jean Marie Ntagwabila.

0 maoni:

Post a Comment