Hatimaye Anderson anaweza kuondoka Old Trafford
KIUNGO
wa Manchester United asiyekuwa fiti, Anderson anaingia kwenye
mazungumzo ya kumaliza maisha yake ya soka Old Trafford na kurudi kwao
Brazil.
Klabu
ya Internacional ya Brazil imeshawasiliana na United pamoja na
wawakilishi wa mchezaji ambapo mazungumzo zaidi yamepangwa kuanza leo
ijumaa asubuhi.
Anderson
hana nafasi katika kikosi cha Louis Van Gaal na hata wakati wa David
Moyes alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina.
Anderson, hajawahi kucheza tena tangu alipoingia dakika 20 za mwisho dhidi ya Burnley mwezi wa nane mwaka jana na sasa anauzwa.
Nyota huyo
mwenye miaka 26 hajaonesha thamani yake tangu alipotua Old Trafford
kutokea Porto sambana na Nani kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 26
mwaka 2007.
Anderson anaelekea kumaliza mkataba wake na United wanafikiria kuuvunja, lakini Internacional wanaweza kukubali kumnunua.
0 maoni:
Post a Comment