YANGA SC imeendelea kujifua kujiandaa na mechi ya kesho kutwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam dhidi ya Ndanda fc.
Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema katika mazoezi ya leo, kocha
mkuu wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ameendelea kufanyia marekebisho
safu yake ya kiungo na ushambuliaji.
“Tunafanya mazoezi kwa siku
kadhaa, nadhani kesho mwalimu atakamilisha programu yake kabla ya mechi
ya jumapili, tunaenda kucheza na Ndanda yenye morali kubwa”.
“Wametoka kushinda na Kagera Sugar, nasisi tuliwafunga Polisi Morogoro, kwahiyo tutaingia kwa tahadhari kubwa”
0 maoni:
Post a Comment