Tumeona baadhi ya wasanii ambao bado wapo kwenye masomo lakini wakifanya kazi zao za muziki akiwemo, Stereo, M Rap Lion, Ben Pol, Nikki wa Pili na wengineo, sasa goodnews ninayokusogezea ni hii kutoka kwa mkali wa Hiphop kutoka ROCK CITY Mwanza, Young Killer ambaye kwa mwaka 2015 amesema atajikita zaidi katika masomo yake.
Akiongea na millardayo.com rapper huyo amesema; ‘Nadhani
utakuwa ni mwaka mzuri pia wa kuendeleza masomo yangu kwasababu mwaka
jana niliwahidi watu na nirudi kweli ila kuna vitu kidogo viliingiliana
ikabidi ni stop ila mwaka huu nina plan za kurudi shule.
Nadhani
inaweza ikawa mwezi wa tano inshallah mwenyezi mungu akibariki kwa sasa
hivi najaribu kuweka mipango sawa, sababu zilizopelekea ni mambo ya
kazi zangu yalikuwa yanaingiliana… nikafanya kazi nikusanye pesa ili
niweze kujisomesha, mwaka huu kazi nitakuwa nafanya ila nitabase sana
kwenye masomo zaidi”–Young Killer.
0 maoni:
Post a Comment