Msanii wa muziki Linex Sunday Mjenda amefunguka na kusema kesho Jan 31 anatarajia kuingia location kufanya maandalizi ya video mpya ya single yake iitwayo Salima aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Akiongea na millardayo.com alisema; ‘Kesho
Jumamosi nitaanza ku shoot video ya wimbo wangu unaitwa Salima
nimefanya na Diamond Platnumz, Salima ni wimbo fulani ambao ukiusikiliza
vizuri una mafunzo ndani yake.
Ni
wimbo ambao tumemuimbia mwanamke ambaye alikuwa na maisha mazuri lakini
maisha yalibadilika baada ya wazazi yake kufariki kwa hiyo maisha
yalivyobadilika akajikuta ana watoto watatu wenye baba tofauti bila yeye
mwenyewe kujielewa lakini mwisho wa siku akafikia point akawa ame give
up na ameamua kuishi maisha yake na watoto wake bila kutegemea Mwanaume,
kwa hiyo ni wimbo fulani ambao una mafundisho kwa dada zetu na kaka
zetu.
Tuta
shoot video na director Adam Juma na hatuta shoot video mjini tuta shoot
video kijijini kwa hiyo watu wenye wataona kitu tofauti kutoka kwangu
na kwa Naseeb’--alisema Linex.
0 maoni:
Post a Comment