Jan 30, 2015

NYOSSO AFURAHIA KAZI ALIYOIFANYA DHIDI YA SIMBA



Beki Juma Nyosso wa Mbeya City amesema amefurahishwa na ushindi walioupata dhidi ya Simba lakini pia uwezo aliouonyesha katika mechi hiyo wikiendi iliyopita.


“Unapocheza na timu yako ya zamani lazima uwaonyeshe kuwa bado upo bora kiasi gani,” hiyo ni kauli ya beki wa Mbeya City, Juma Nyosso aliyoitoa baada ya timu yake kuifunga Simba mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, juzi.
Simba ilipata kipigo hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, huku Nyosso ambaye ni beki wa zamani wa Simba akiwa nahodha wa Mbeya City.
“Nimefurahi tumeshinda kwenye mchezo mgumu kama huu na usiotabirika lakini kuhusu kucheza na timu yangu ya zamani ni kitu kizuri zaidi kwa kuwa unapata nafasi ya kuwaonyesha kuwa bado upo bora kwa kiwango gani na nashukuru nimefanikiwa kulifanya hilo.


“Nimewaonyesha viongozi wa Simba kuwa walifanya makosa makubwa ya kuniacha wakidai nimeshuka kiwango,” alisema Nyosso.

0 maoni:

Post a Comment