YANGA yenye kumbukumbu ya ushindi
wa goli 1-0 iliovuna mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Jamhuri
Morogoro dhidi ya Polisi Moro inawania pointi tatu zingine jumapili,
februari 1 mwaka huu itakapocheza na Ndanda fc uwanja wa Taifa Dar es
salaam.
Hiyo itakuwa mechi ya nne ya ligi
kuu kwa kocha Hans Van Pluijm ambaye alianza kwa sare ya mabao 2-2 na
Azam fc Desemba 28 mwaka jana akirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo.
Baadaye akatoka suluhu (0-0) na
Ruvu Shootings, Januari 17 mwaka huu. Mwishoni mwa wili iliyopita
alishinda 1-0 dhidi ya Polisi Moro.
Katika mechi tatu alizocheza na
kushinda moja, Pluijm ameonekana kufanikiwa kuijenga Yanga inayocheza
mpira wa pasi na kushambulia kwa kasi tofauti na kipindi cha Marcio
Maximo ambapo Yanga walikuwa wanajihami sana.
Hata hivyo, bado kikosi hicho
kilichosheheni nyota wengi akiwemo Mliberia Kpah Sherman, Mrundi Amissi
Tambwe, Wanyarwanda Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima, Wazawa Danny
Mrwanda, Saimon Msuva kina mapungufu ya kucheka na nyavu.
Yanga wanatengeneza nafasi
nyingi, lakini umaliziaji ni mbovu na ilifikia hatua uongozi ukaruhusu
baadhi ya wanachama wake kuomba dua la kuondoa nuksi klabuni hapo.
Mbali na mechi hiyo ya jumapili, kesho Jumamosi kuna mechi nyingine zitapigwa.
Simba watawakaribisha JKT Ruvu uwanja wa Taifa, Coastal Union watachuana na Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ruvu Shootings wataikaribisha
Stand United uwanja wa Mabatini, wakati Tanzania Prisons watakuwa
nyumbani uwanja wa Sokoine kuchuana na Kagera Sugar.
Polisi Moro watakabiliana na wababe wa Simba, Mbeya City fc.
Mechi ya Mgambo na Azam fc haitakuwepo kwasababu mabingwa watetezi hawapo nchini kwasasa.
Azam fc ipo nchini DR Congo
kushiriki mashindano ya Mazembe yanayoendelea mjini Lubumbashi ikiwa ni
maandalizi ya mechi ya ligi ya mabingwa itakayopigwa mwezi ujao dhidi ya
El Merreick ya Sudan.
0 maoni:
Post a Comment