Habari zaidi kutoka lubumbashi zinasema kuwa klabu ya CSKA moscow ya Urusi iliamua kuachana na Samatta kwa sasa kwa sababu ya kuumia enka akiwa katika wiki ya kwanza ya majaribio.
kiongozi mmoja wa mazembe ambaye hakupenda kutajwa jina alisema kuwa timu hiyo ya ulaya ilivutiwa na mchezaji huyo wa Tanzania lakini ilishindwa kumtathimini zaidi baada ya kuumia.
Hata hivyo amesema kuwa klabu hiyo (TP MAZEMBE) ipo bega kwa bega na mchezaji huyo ili kutimiza azma yake ya kucheza ulaya.
Samatta ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Tp mazembe tangu asajiliwe kutoka simba ya Dar es salaam, alipania mno mwezi huu january kuamia ulaya lakini inaonekana wakati wake bado.
0 maoni:
Post a Comment