Juan Cuadrado aliyepigwa picha akishangilia baada ya kuifungia Fiorentina mapema mwezi huu yuko mbioni kutua Chelsea
NYOTA
wa kombe la dunia wa Colombia, Juan Cuadrado yuko mbioni kusajiliwa na
Chelsea kwa dau la paundi milioni 26.8 na tayari Jose Mourinho anataka
kulazimisha dili hilo kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa
jumatatu.
Kulikuwa
na ripoti nyingi kutoka Chelsea, lakini winga huyo wa Colombia anatua
darajani wakati huu Andre Schurrle amejiunga na timu ya Ujerumani ya
Wolfsburg kwa ada inayokaribia paundi milioni 30.
Mourinho
alitumaini kumsajili Cuadrado kabla ya mechi ya kesho ya ligi kuu dhidi
ya Manchester City katika uwanja wa Stamford Bridge, lakini mazungumzo
ya Schurrle yamekwamisha mpango.
0 maoni:
Post a Comment