Bayern Munich wameacha na mpango wa kumsajili Marco Reus
Bayern
Munich wameachana na mbio za kumsajili Marco Reus na kuacha milango
wazi kwa klabu ya Real Madrid na klabu kubwa za ligi kuu England.
Bayern
wamefikia maamuzi ya kutomshawishi Reus wiki kadhaa zilizopita kwa
madai kuwa tayari wana viungo washambuliaji wengi na hawataki kuharibu
uhusiano wao wa karibu na Borussia Dortmund, hii ni kwa mujibu wa gazeti
la Bild.
Real
wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Reus, lakini kutokana na tetesi za
klabu za Hispania kufungiwa usajili, anaweza kutua katika timu za ligi
kuu England majira ya kiangazi mwaka huu.
Reus ni miongoni mwa wachezaji wakubwa barani ulaya na atazivutia klabu kubwa.
Taarifa za
Bayern kutomsajili zitawashitua Manchester City na Chelsea ambao
wanaendelea kutumia pesa kuimarisha vikosi vyao ili kufikia ubora mkubwa
wa ulaya.
0 maoni:
Post a Comment