Suala la mshambuliaji wa
Simba, Elius Maguri kufanyiwa vitendo vya udhalilishwaji vimepingwa kwa nguvu
zote na uongozi wa Simba.
Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza
Aveva kitendo alichokifanya beki Juma Nyosso dhidi ya Maguri kumshika makalio
na kumdhalilisha kwa kumuingiza kidole lilikuwa jambo si la kiungwana.
Nyosso alifanya kitendo
hicho cha kulaaniwa katika mechi ya
Ligi Kuu Bara Kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar.
Gazeti
maarufu la michezo nchini la Championi, limechapisha picha ikimuonyesha
Nyosso akifanya vitendo hivyo vya udhalilishaji dhidi ya Maguri, kitu
ambacho wadau wengi wamelaani na kusema Nyosso hakustahili kufanya
hivyo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar, Aveva alisema Maguri ambaye amejiunga na Simba msimu huu
akitokea Ruvu Shooting, alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji na kuitaka TFF
kuchukua hatua za kisheria dhidi kwa Nyosso aliyewahi kuichezewa Simba.
“Kuhusiana na suala la
tukio hilo kuchapishwa kwenye gazeti la Championi kwamba ni sawa au la,
kitaaluma mimi si mtaalamu wa masuala ya habari, lakini tutalijadili na
wenzangu.
“Lakini la msingi ninaloweza
kusema ni kwamba kitendo alichofanyiwa Maguri si sawa kabisa na tunakikemea
vikali, kwani tumesikitishwa sana.
“Pia hii ni changamoto wa viongozi
wa klabu na shirikisho. Kwamba huu ndiyo wakati wa kwenda na teknolojia.
Tusikatae kw akuwa mambo ndivyo yalivyo.
“Angalia suala la Suarez
alipomng’ata mchezaji wa Italia,
Fifa ilimfungia baada ya kutumia teknolojia na haikutumia ripoti ya waamuzi
pekee, hivyo na sisi umefika wakati wa kuheshimu teknolojia kwa ajili ya kukomesha
vitendo kama hivyo ambavyo tayari vimejionyesha kwa Tambwe, Okwi na Maguri,
lakini pia huko daraja la kwanza ndiyo usiseme,” alisema Aveva.
Aidha, Aveva alivishukuru
vyombo vya habari kwa kuendelea kuibua mfululizo matukio mabaya ya ukatili na
udhalilishaji katika soka ili kuonyesha hali halisi.
0 maoni:
Post a Comment