Jan 30, 2015

OKWI KAMILI GADO KUWAVAA JKT RUVU KESHO TAIFA


s4
KIUNGO mshambuliaji wa Simba Sc, Mganda Emmanuel Anord Okwi anatarajia kuivaa JKT Ruvu kesho uwanja wa Taifa katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita akiwa uwanja wa mazoezi wa JKT Mbweni ambapo Simba inaendelea na mazoezi hivi tunavyoongea na kueleza kuwa Okwi yuko fiti na atacheza mechi ya kesho.
“Nipo hapa uwanjani JKT Mbweni, Okwi anaendelea na mazoezi. Kesho atacheza”. Amesema Nyasio.
Pia Nyasio amesema beki wa pembeni Hassan Ramadhan Kessy yuko fiti kucheza kesho na muda huu unaendelea  na mazoezi.
Hata hivyo, Afisa habari huyo amesema Simba itaendelea kuikosa huduma ya kiungo Said Hamis Ndemla ambaye bado anasumbuliwa na majeruhi.
Okwi, Ndemla na Kessy waliikosa mechi ya jumatano iliyopita uwanja wa Taifa ambapo Mnyama Simba alichapwa 2-1 na Mbeya City.
Nyasio amesema kesho watapambana kupata ushindi, licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto katika michuano ya ligi kuu.

0 maoni:

Post a Comment