Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema unatarajia kuwasilisha barua kwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jumatatu ijayo kuomba mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar wa
Februari 8, usogezwe mbele.
Yanga
inatarajiwa kukipiga na BDF XI ya Botswana katika Kombe la Shirikisho mnamo
Februari 14 lakini inatakiwa itekeleze majukumu yake katika Ligi Kuu Bara,
Februari 8.
Katibu
wa Yanga, Jonas Kiboroha amesema hii: “Tumeandaa barua ambayo tutaipeleka TFF
siku ya Jumatatu kuomba mchezo wetu dhidi ya Mtibwa usogezwe kwa lengo la
kupata muda wa kujiandaa kabla ya kuivaa BDF XI.”
Wakati huohuo,
Yanga ipo katika mazungumzo na timu ya Vipers ya Uganda kwa ajili ya kucheza
nao mchezo wa kirafiki kabla ya kuvaana na BDF XI.
Mkuu
wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, ndiye aliyetoa tamko kwa kusema: “Tupo
katika mazungumzo na Vipers lakini hatuwezi kusema lini tutacheza nao rasmi kwa
kuwa bado mazungumzo yanaendelea.”
0 maoni:
Post a Comment