Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameuomba uongozi wa timu hiyo umpunguzie majukumu au umuache ende zake.
Matola ameuambia uongozi wa Simba kwamba ana mambo ya kifamilia yanayomkabili hivyo asingeweza kupambana na presha inayoendelea.
Rais wa Simba, Evans Aveva amesema tayari Matola amewaambia kwa mdomo kuhusiana na hilo na sasa wanalishughulikia.
"Ni kweli amesema hivyo, sasa nimemwambia aandike barua kuhusiana na alichosema," alisema Aveva.
"Baada ya hapo tutakutana na kukaa ili kujua cha kufanya kuhusiana na suala hilo," aliongeza Aveva.
Simba ilipoteza mechi yake ya pili ilipokutana na Mbeya City na kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar,Jumapili.
Hali ambayo imeamsha jazba kwa mashabiki wa Simba ambao asilimia kubwa waliangua kilio.
0 maoni:
Post a Comment