Uongozi wa Yanga SC umewapa pole
watani waowa jadi, Simba baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City
katika mechi yao iliyopita.
Simba SC iliyokosa huduma ya nyota wake Mganda Emmanuel Okwi,
ilipata kipigo hicho cha pili msimu huu na cha kwanza kwa kocha mkuu
mpya, Mserbia Goran Kopunovic katika mechi yao ya kiporo ya raundi ya 10
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa jijini hapa
jana.Baada ya kichapo hicho, Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasiliano ya Yanga, Jerry Muro, alisema jana kuwa: “Tunawapa pole wenzetu wa upande wa pili (Simba) kwa kupata pancha leo (juzi). Tunaamini wataziba na kurejea katika mapambano.”
Yanga SC na Simba SC zimekuwa timu pinzani tangu hata kabla ya kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 1965, Timu hizo zilianzishwa 1935 na 1936, Yanga SC ikiwa ni ya kwanza.
0 maoni:
Post a Comment