Jose Mourinho na Diego Costa wakizungumza wakati wa mechi dhidi ya Liverpool
Jose
Mourinho amenuna baada ya chama cha soka England, FA kusema kinamtoza
faini Diego Costa kwa kuonesha mchezo usiokuwa wa kiungwana.
Mourinho
ameichukia FA na anaamini mfungaji wake anayeongoza kufumania nyavu
ametolewa kama mbuzi wa kafara kufuatia kumchezea vibaya beki wa
Liverpool, Emre Can.
Kocha
huyo wa Chelsea ambaye amewahi kutozwa faini na FA alitakiwa kuwa na
mkutano na waandishi wa habari kesho ijumaa kuelekea mechi ngumu dhidi
ya Manchester City jumamosi, lakini ameufuta.

Diego Costa alionekana kumkanyaga mguu wa kulia Emre Can kwenye mechi ya nusu fainali ya Capital One dhidi ya Liverpool

Costa anaweza kufungiwa mechi tatu baada ya kutozwa faini na FA kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Can.
Klabu ya
Chelsea imefuta ratiba ya mkutano na waandishi wa habari na
hatawathubutu hata kumtuma kocha msaidizi, Steve Holland kuzungumza na
vyombo vya habari.
Imethibitishwa kuwa kikao cha nidhamu cha FA kitakachokaa kesho kitamuadhibu Costa.
Licha ya
Costa kukataa kosa lake, mshambuliaji huyo wa Chelsea anatarajia
kufungiwa mechi tatu kuanzia ya jumamosi dhidi ya Man City.
0 maoni:
Post a Comment