Ingawa ni mazoezi lakini ushindani mkali kati ya beki Mganda, Juuko Murishid dhidi ya Mghana, Aboagye Nelson haikuwa kazi ndogo.
Katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam (UDSM), Aboagye
ambaye anafanya majaribio Simba akiwaniwa kusajiliwa, alikuwa akijaribu
kuonyesha uwezo wake kwa kuwatoka mabeki mara kadhaa.
Hali hiyo
ilionyesha kutokubalika kwa Murishid, ambaye alikuwa akipambana naye vilivyo
utafikiri ni mechi.
Hali hiyo
iligeuka kuwa burudani kwa wengine huku Mghana huyo naye akionekana kuwa mbishi
ile mbaya.
0 maoni:
Post a Comment